wenye ulemavu wa macho
na Viziwi iliyoandaliwa na Taasisi ya Mpango wa Usalama Barabarani (TARSI).
WATU wenye ulemavu wa macho wamesema wanapata shida kutumia barabara kwa kuwa wengi wao hawana elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara.Aidha wamesema kundi hilo limekuwa halipewi kipaumbele kuhusu elimu za namna ya kutumia barabara jambo linalofanya wengi wanapoteza maisha.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mlezi wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB) James Shimwenye, katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Mpango wa Usalama Barabarani (TARSI).
Amesema miongoni mwa changamoto wanazo kutananazo wasioona ni pamoja na kushindwa kutambua wakati upi ni sahihi kuvuka barabara, sehemu salama ya kuvukia na namna ya kutambua taa nyekundu na za kijani zinapokuwa zimeruhusu.
“Changamoto za vyombo vya usafiri kutosimama vizuri katika vituo jambo ambalo husababisha usumbufu wakati wa kupanda na kushuka kwa watu wenye ulemavu.
“Kutotambuliwa kwa fimbo nyeupe kama alama yetu na hivyo husababisha tukae muda mrefu barabarani ili tuweze kuvuka. Ukosefu wa elimu ya usalama barabarani miongoni mwa changamoto kubwa bila kupoteza muda tunaiomba serikali ituandalie mpango maalumu wa mafunzo ya muda mrefu ili kutuokoa” amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa (TARSI) Maliki Barongo amesema taasisi yao inajihusisha na utoaji wa elimu bararabani kwa lengo la kuisaidia serikali katika kupunguza ajali.
Amesema Pia huwa wanaandaa mafunzo kwa wajenzi wa barabara ili waweze kujenga barabara rafiki na zisaidie kupunguza ajali vilevile kwa watumiaji wa barabara.
“Sisi tumeona kuna haja ya kuandaa mafunzo kwa wenye ulemavu wa macho kwa lengo la kuwajengea uwezo tumeona mara kadhaa kundi hili kama limesahaulika.
“Huwezi kuwaweka katika kundi la watembea kwa miguu kwa sababu tayari wao wana ulemavu, wa macho lengo wajue wajibu wao na watambue sheria za usalama barabarani.
“Kwahiyo hii elimu wakiipata hawa na madereva wengine itasaidia kupunguza ajali za barabarani ninaomba niwasihi ninyi ndio mabalozi elimu mliyoipata iwafikie na watu wengine ambao hawajafika katika semina hii” amesisitiza Barongo mbele ya umati wa walemavu wa macho walikuwa wamefika kuhudhuria mafunzo hayo
Barongo amesema kila mmoja anafahamu madhara ya ajali ikiwamo kupoteza maisha kupata ulemavu wa kudmua na kuongeza utegemezi kwa familia na taifa.
Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Upande wa Usalama Barabarani wa kutoka Makao Makuu ya Trafiki Dar es Salaam, SSP Mbunja Matibu amesema amefurahi TARSI, kumkutanisha na kundi hilo na kwamba elimu waliyoipata anaamini itasaidia kuwafanya wawe na matumzii sahihi na salama ya barabara.
Amesema itawasaidi kuchukua tahadhari na watu ambao huwa wana waongoza. “Madereva wa vyombo vya moto wanapoona alama za barabarani au mtu mwenye changamoto ya ulemavu watoe kipaumbele kwa kupunguza mwendo au ikiwezekana wasimame ili wasiwasababishie madhara.
Amesema mkakati wao ni kuendelea kutoa elimu maeneno mbalimbali nchini na ndio maana alipopata mwaliko wa kukutana na kundi hilo hakusiata kwa sabbau usalama barabarani jukumu la wote.
Kuhusu wanaopuuza alama za barabarani alisema kazi yao ni kusimamia sheria na kuwakumbusha wahusika kwa kuweka alama za barabarani.
Nao wenye ulemavu wa macho kwa pamoja walisema hawajawahi kupata elimu ya usalama barabarani na hivyo wengi wanatumia barabara kwa hisia jambo ambalo wakati mwingine huwasababishia ajali

